Connect with us

Makala

Simba sc Kuwakosa Watatu Singida

Kocha wa klabu ya Simba sc Juma Mgunda amesema jumla ya mastaa watatu wa kikosi cha kwanza watakosekana katika mchezo wa kesho dhidi ya Singida Big Stars utakaofanyika katika uwanja wa Liti mkoani Singida.

Mgunda amesema hayo wakati akizungumza na wanahabri katika mkutano maalumu kuelekea mechi hiyo ambayo hufanyika siku moja kabla ya mchezo kwa mujibu wa kanuni za ligi kuu nchini.

Mastaa Cletous Chama,Augustine Okrah,Israel Mwenda na Nelson watakosekana katika mchezo wa kesho kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo majeraha na kufungiwa ambapo Chama amefungiwa na Bodi ya ligi kwa kosa la kutosalimiana na wenzake wa Yanga sc katika mchezo uliozikutanisha timu hizo Oktoba 23 mwaka huu.

Kocha Juma Mgunda amelalamika hasa kukosekana kwa Chama akisema kuwa adhabu hiyo imechelewa kutangazwa ambapo tayari alikua ameshamuweka katika mipango yake ya mchezo wa kesho ilhali mamlaka ilikaa na taarifa hiyo tangu Novemba 4 na kuja kuitoa siku moja kabla ya mchezo kitu ambacho sio sahihi kwa upande wake.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala