Connect with us

Makala

Simba sc Kushiriki Super League

Mabingwa wa soka nchini kwa miaka minne mfululizo iliyopita klabu ya Simba sc ni timu pekee kutoka ukanda wa Afrika Mashariki ambayo imepata nafasi ya kushiriki michuano ya Super League ambayo inajumuisha timu vigogo barani Afrika.

Michuano imepangwa kuanza msimu wa mwaka 2023 ambapo hivi leo imepitishwa rasmi na mkutano mkuu wa Shirikisho la soka barani Afrika (Caf) ambalo linafanya mkutano wake mkuu nchini kuanzia hivi leo unaofanyika jijini Arusha.

Moja ya ajenda ya mkutano huo ilikua ni suala hilo la kuwa na ligi yenye pesa ndefu ambayo itashirikisha timu vigogo 24 barani Afrika huku Simba sc ikifanikiwa kuingia kwa kushika nafasi ya 14 barani Afrika kwa ubora.

Aidha kuhusu michuano hiyo bingwa atapata kiasi kikubwa cha pesa ambacho ni takribani zaidi ya bilioni 200 huku kila klabu ikipewa kiasi cha bilioni tano za maandalizi ya michuano hiyo pekee ambapo zaidi ya bilioni mia mbili za kitanzania zitatumika katika michuano hiyo ikiwemo kuyapatia mashirikisho ya soka kwa nchi wanachama kiasi cha zaidi ya Bilioni 2 za kitanzania kwa ajili ya miradi mbalimbali ya soka.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala