Connect with us

Makala

Simba sc Kupasha kwa Pan African

Kikosi cha klabu ya Simba siku ya kesho Septemba 26 kitacheza mechi ya kirafiki dhidi ya Pan African FC inayoshiriki ligi daraja la kwanza nchini kwa lengo la kujiweka sawa kwa ajili ya michuano ya kimataifa.

Huu unakuwa mchezo wa kwanza wa kujiweka sawa kwa Simba sc kabla ya mchezo wa marudiano dhidi ya Power Dynamos ya Zambia katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika utakaochezwa Oktoba 01, katika Uwanja wa Azam Complex Chamazi jijini Dar es salaam.

Mchezo huo utachezwa saa 3 asubuhi katika uwanja wa Mo Simba Arena Bunju ambapo baadhi ya mastaa wa klabu hiyo wanatarajiwa kucheza hasa wale wanaokaa benchi ili kuangalia viwango vyao kuamua nani aingie katika kikosi cha kwanza.

Simba sc inapaswa kuwa fiti kuelekea katika mchezo wa marudiano dhidi ya Power Dynamos utakaofanyika mwishoni mwa wiki hii ambapo matokeo ya sare ama ushindi utawapa tiketi ya kufuzu hatua ya makundi ya klabu bingwa barani Afrika.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala