Connect with us

Makala

Simba Sc Kuifuata Al Masry Alfajiri

Msafara wa kikosi cha timu ya Simba sc kijatarajiwa kuondoka alfajiri ya kesho Machi 28 kuelekea nchini Misri kwa ajili ya mchezo wa kombe la shirikisho barani Afrika dhidi ya Al Masry.

Mchezo huo unaotarajiwa kufanyika April 2 2025 nchini humo ambapo mshindi atasubiri mchezo wa marudiano jijini Dar es Salaam April 9 2025 ili kupata tiketi ya kufuzu nusu fainali.

Msafara rasmi wa klabu ya Simba Sc utakaokua na mastaa utaondoka nchini Alfajiri ambapo pia kipa Moussa Camara amejumuishwa katika masafara huo huku beki Che Fondoh Malone akiwa hayumo katika orodha ya mastaa wanaosafiri na timu hiyo.

Msafara huo unajumuisha pia mastaa walioko nchini Misri moja kwa moja ambapo wao walitokea nchini Morocco walipokua na kambi ya timu ya Taifa Stars na wameunganisha moja kwa moja nchini Misri.

Mastaa hao ni Ally Salim,Shomari Kapombe,Abdulrazack Hamza,Yusuph Kagoma,Mohamed Hussein na Kibu Dennis.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala