Connect with us

Makala

Simba “Out” Caf

Klabu ya Simba sc imeshindwa kutimiza ndoto yake ya muda mrefu ya kucheza hatua ya nusu fainali ya michuano ya klabu bingwa barani Afrika baada ya kupoteza mchezo dhidi ya Wydad Ac katika hatua ya robo fainali nchini Morocco kwa penati 4-3.

Awali Simba sc ilishinda kwa 1-0 katika mchezo wa kwanza hapa nchini na kwenda ugenini ikiwa na mtaji wa bao moja lakini mapema kipindi cha kwanza Wydad walisawazisha bao hilo kupitia kwa mshambuliaji wao nguli Bouly Sambou dakika ya 24 kwa kichwa baada ya mabeki wa Simba sc kuzembea kuokoa mpira wa juu.

Kuingia kwa bao hilo kuliufanya mchezo kuwa wa kuviziana huku kila timu ikiwa makini kutafuta bao lakni mpaka dakika tisini zinamalizika mchezo ulikua 1-0 na kufanya matokeo ya jumla kuwa 1-1 ambapo kwa mujibu wa kanuni ilibidi mikwaju wa penati iamue mchezo huo.

Shomari Kapombe na Cletous Chama walikosa mikwaju yao huku Erasto nyoni na Saido Ntibanzokiza walifanikiwa kufunga na upande wa wenyeji walipata penati zote nne huku kipa wao akiokoa penati hizo mbili na mchezo kumalizika kwa Wydad kufuzu huku wakisubiri mshindi kati ya Mamelod Sundowns na Cr Belouzdad katika hatua ya nusu fainali.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala