Connect with us

Makala

Simba Day Yafunika

Lile tamasha kongwe la michezo lililokua likisubiriwa kwa hamu na mashabiki wa klabu ya Simba sc sambamba na wadau wa michezo nchini limefanyika jana kwa kufana hasa mgeni rasmi Rais Samia Suluhu Hassan ambaye ilikua ni mara yake ya kwanza kuhudhuria tukio la klabu hiyo tangu aingie madarakani.

Tamasha hilo lilifanyika katika uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es salaam ambapo Idadu kubwa ya mashabiki waliojitokeza kuhudhuria tamasha hilo imekua kivutia barani Afrika ambapo kwa mujibu wa kampuni ya N-card ambayo inajihusisha na uuzaji wa tiketi za kuingilia uwanjani jumla ya mashabiki 58 na zaidi walinunua tiketi.

Kwa upande wa Burudani msanii Ali kiba alipamba tamasha hilo kwa nyimbo zake kali na za kusisimua huku pia msanii Tundaman naye akishiriki sambamba na wasanii wengine.

Kivutia kingine ni Meneja wa Idara ya Habari ya klabu hiyo Ahmed Ally ambaye yeye aliingia kwa kutimia ngamia na kuwafurahisha mashabiki wa klabu hiyo hasa wakati wa utambulisho wa wachezaji wa klabu hiyo ambapo mastaa kama Cletous Chama,Fabrice Ngoma na Aishi Manula walishangiliwa na mashabiki.

Mchezo baina ya Simba sc na Power Dynamos ya Zambia ulimalizika kwa matokeo ya 2-0 ambapo magoli ya Simba sc yalifungwa na Leandre Onana na Fabrice Ngoma ambao pia viwango vyao viliwakosha mashabiki wa klabu hiyo japo mastaa kama Luis Miqquisone na Abdalah Khamis walionekana hawana uimara wa mwili.

Mastaa wenyeji kama Cletous Chama,Saido Ntibanzokiza na Kibu Dennis walionyesha nguvu kubwa ya kupambana huku wakiwa na utimamu wa mwili wa kutosha sambamba na Mzamiru Yassin huku beki Che Fondoh Malone akionyesha uwezo wa hali ya juu.

Simba sc sasa baada ya tamasha hilo wanatarajiwa kusafiri kuelekea jijini Tanga kuwavaa Singida Big Stars kwa ajili ya mchezo wa kombe la Ngao ya Hisani utakaofanyika katika uwanja wa Mkwakwani siku ya alhamis.

 

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala