Connect with us

Makala

Simba Day Full House

Klabu ya Simba sc imetangaza kuuza tiketi zote za tamasha lake la kila mwaka la Simba day litakalofanyika siku ya jumapili katika uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es salaam ambapo kutakua na burudani tofauti tofauti sambamba na mechi dhidi ya Power Dynamos ya Zambia.

Simba sc iliweka kiingilio cha chini cha Tsh 5000 huku kiingilio cha juu kikiwa ni laki mbili ambapo tiketi hizo sasa zimeisha baada ya mashabiki kuzinunua zote.

Simba sc imekua na kawaida ya kupata mwitikio mkubwa katika miaka ya hivi karibuni katika tamasha hilo japokua kwa misimu miwili iliyopita hawakufanikiwa kujaza uwanja katika majukwaa yote.

Kuisha kwa tiketi hizo kumeweka rekodi hapa nchini katika matamasha ya michezo kwani haijawahi kutokea kwa klabu ya mpira kumaliza tiketi siku tatu kabla ya tamasha lenyewe.

Mwitikio wa mashabiki umekua mkubwa kutokana na usajili wa baadhi ya mastaa kikosini humo huku wakiwa hawajaonekana tangu wasajiliwe klabuni hapa ambapo mastaa kama Luis Miqquisone,Fabrice Ngoma,Andre Onana na Che Fondoh Malone wamekua kivutio kikubwa mtandaoni.

Pia aina ya promesheni kuelekea mchezo ilivyofanya na idara ya habari ya Simba sc imekua yenye ubunifu wa kipekee ambapo kitendo cha kuzindulia jezi katika kilele cha mlima Kilimanjaro ikiwa pia ni sababu iliyoipa thamani zaidi tamasha hilo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala