Connect with us

Makala

Shangwe la Bongo Lawakuna Us Monastr

Rais wa klab ya US Monastir ya nchini Tunisia Ahmed Belli atoa pongezi kwa Yanga SC na mashabiki wake baada ya jana kupokea ‘kichapo’ cha mabao 2-0 kutoka kwa vinara hao wa NBC Premier league Yanga sc kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho barani Afrika.

Rais huyo alizungumza hayo mapema leo baada ya timu yake kuingia makubaliano na Singida Big Stars kwa ajili ya kushirikiana masuala mbalimbali ya soka ambapo alionekana kushangazwa na mzuka na shangwe za mashabiki wa soka nchini walizoonyesha katika mchezo huo kiasi cha kupoteza kwa mabao 2-0.

Singida Big Stars na klabu hiyo zimeingia makubaliano ya ushirikiano katika masuala mbalimbali ya soka katika maeneo ya ufundi,miundombinu na maendeleo kwa ujumla wake.

Singida Big Stars ina uhakika wa mwakani kushiriki michuano ya kimataifa baada ya kuwa na uwezekano mkubwa wa Tanzania kuingiza timu nne katika michuano ya kimataifa.

 

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala