Connect with us

Makala

Semedo Atimkia Wolves

Beki wa kulia ambaye pia ni raia wa Ureno,Nelson Semedo ametua Wolverhampton Wanderers kwa mkataba wa miaka mitatu akitokea Barcelona.

Kocha wa Wolves,Nuno Espirito Santo amefurahi kutua kwa beki huyo kwani amekuwa akimsaka beki wa kujaza nafasi ya Matt Donerty aliyetua Tottenham mwezi uliopita.

Semedo ametua Wolves kwa kima cha bilioni 5.2 ambapo anakuwa mwanasoka ghali kusajliwa na klabu hiyo  baada ya Silva aliyehudumiwa kwa Bilioni 4.9.

Usajili wa Semedo unakuwa wa tatu kwa Wolves tangu dirisha kubwa la usajili kufunguliwa ambapo wawili ni Fabio Silva akitokea Fc Porto na Ki-Jana Hoever akitokea Liverpool.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala