Connect with us

Makala

Samia Aipongeza Serengeti Girls

Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh.Samia Suluhu Hassan ameipongeza timu ya Taifa ya wanawake chini ya miaka 17 Serengeti Girls baada ya kufanikiwa kufuzu hatua ya robo fainali ya kombe la Dunia la wanawake chini ya umri wa miaka 17 linaloendelea nchini India.

Serengeti Girls ambayo ilipangwa katika kundi sambamba na timu za Japan,Ufaransa na Canada imefanikiwa kufuzu baada ya kumaliza katika nafasi ya pili nyuma ya Japan waliomaliza kinara wa kundi ambao Serengeti Girls imefuzu baada ya kupata alama nne ikiifunga Ufaransa na kutoa sare na Canada baada ya kufungwa mabao 4-1 na Japan katika mchezo wa kwanza.

Kutokana na kufuzu katika hatua hiyo sasa Serengeti Girls itavaana na Colombia mchezo utakaochezwa siku ya Jumamosi Oktoba 22 jijini Goa nchini India yanakofanyika mashindano hayo.

‘Mmenifurahisha sana Watoto wangu @serengetigirls kwa kuandika historia ya kufuzu kuingia robo fainali ya Michuano ya Kombe la Dunia kwa Wanawake chini ya miaka 17 nchini India. Mmefanya jambo kubwa kwa nchi yetu Tanzania na nawatakia kheri katika hatua ya robo fainali.” Rais Samia Suluhu Hassan ameandika kupitia ukurasa wake wa twitter.

Akizungumza mara baada ya mchezo kumalizika, Mhe Gekul ameishukuru Serikali chini ya Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha timu hiyo ya Serengeti kuanzia kuweka Kambi ya kutosha katika Mji wa Southampton nchini Uingereza ambapo ilifanya maandalizi mazuri ambayo yameifikisha hapo timu hiyo.

“Nawapongeza sana wanangu hawa, wameliheshimisha Taifa, wameitangaza Tanzania, sasa hivi sio Royal Tour peke ake inayoweza kuitangaza nchi yetu bali hata Sekta ya michezo imeiweka Tanzania kuwa miongoni mwa nchi zenye vipaji na kujulikana zaidi” amesema Mhe. Gekul.

 

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala