Connect with us

Makala

Salah Aingoza Misri Nusu Fainali

Timu ya Taifa ya Misri imefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali baada ya kuifunga Morroco mabao 2-1 katika mchezo mkali wa hatua ya Robo fainali uliofanyika katika uwanja wa Ahmadou Ahidjo Stadium uliopo jijini Younde nchini Cameroon.

Morroco walitangulia kwa bao la mapema dakika ya saba kwa penati iliyofungwa kiufundi na Sofiane Boufal na bao hilo lilidumu mpaka mapumziko huku dakika nane baada ya kurudi kipindi cha pili nahodha Mohamed Salah alisawazisha bao hilo ambalo lilipelekea dakika 90 za mchezo kumalizika timu hizo zikiwa sare.

Dakika za nyongeza ziliyoyoma na ndipo dakika ya 100 kati ya 120 za nyongeza Mohamed Trezeguet alifunga bao la pili kwa Misri ambalo lilidumu mpaka mwisho wa mchezo na kuwafanya Misri kufuzu hatua ya nusu fainali ambapo watakutana na wenyeji Cameroon ambapo watachuana siku ya alhamis kupata mshindi atakayekwenda fainali.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala