Connect with us

Makala

Saido Atemwa Burundi

Kocha Mkuu wa Burundi ‘Intamba Mu Rugamba’, Etienne Ndayiragije amemwaacha nje ya kikosi kiungo wa Simba SC, Saido Ntibazonkiza wakati Burundi ikijiandaa kukabiliana na Namibia kwenye michezo ya kufuzu Afcon 2023 nchini Ivory Coast mwezi ujao.

Saido anatuhumiwa kwa utovu wa nidhamu baada ya kukataa kushiriki mchezo wa kirafiki dhidi ya Indonesia mapema mwezi Machi mwaka huu.

Mlinda mlango wa Coastal Union Justin Ndikumana ameitwa kikosini humo akiwa ni mchezaji pekee kutoka nchini kwa mastaa wanaocheza ligi kuu ya Nbc.

Saido amekua na matatizo ya mara kwa mara ya kinidhamu ambapo hata alipokua na Yanga sc alitemwa katika kikosi hicho baada ya kukutwa na utovu wa nidhamu kuelekea mchezo wa nusu fainali ya kombe la shirikisho dhidi ya Simba sc.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala