Connect with us

Makala

Sababu Kifo cha Sonso

Mchezaji wa zamani wa klabu ya Yanga sc Ally Sonso amefariki dunia tarehe 11/2/22 jioni katika hospitali ya Muhimbili alipokua akipatiwa matibabu ya mguu ambao ulianza kumsumbua mwaka jana mwezi novemba jijini Mwanza.

Inasemekana kua mchezaji huyo alikua fiti kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa timu yake ya Ruvu shooting mpaka masaa macheche kabla ya mchezo kujiskia maumivu makali ya mguu uliomfanya kushindwa kucheza mchezo huo huku mguu ukianza kuvimba na kuwa kama Tende.

Kwa mujibu wa taarifa ya Masau Bwire ambaye ni msemaji wa klabu ya Ruvu Shooting kuwa mchezaji huyo aliunganishwa na daktari wa timu ambaye alikua akifuatilia matibabu yake mpaka alipoomba kwenda kujiuguza nyumbani.

Inasemekan kwamba mguu huo ulimsumbua mchezaji huyo mpaka ulipovimba na kuanza kutoa vidonda ndipo alipopelekwa hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambapo alipatiwa matibabu mpaka alipoomba kwenda kujiuguza nyumbani tena lakini alizidiwa na kurudishwa hospitalini kisha kulazwa na ndipo mauti yalipomkuta.

Sonso aliwahi kuvitumikia vilabu vya Yanga sc,Lipuli Fc ya Iringa na mpaka anafariki alikua mchezaji wa klabu ya Ruvu Shooting huku akitarajiwa kuzikwa siku ya tarehe 13 mwezi huu.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala