Connect with us

Makala

Real Madrid Yatinga Fainali Uefa

Ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya klabu ya Manchester City ilioupata klabu ya Real Madrid umeiwezesha kuingia hatua ya fainali ya michuano ya klabu bingwa barani ulaya katika mchezo uliofanyika Santiago Bernabeu jijini Madrid.

Katika mchezo wa awali jijini Manchester,Real Madrid ilipoteza kwa mabao 4-3 hivyo kulazimika kuibuka na ushindi katika mchezo wa marudiano ambao imefanikiwa kufuzu kwa ushindi wa jumla wa 6-5 huku ikijiandaa kuwavaa Liverpool katika mchezo wa fainali utakaofanyika Paris Ufaransa.

Riyad Mahrez aliwapatia City bao la uongozi dakika ya 73 na kuongeza presha kwa kocha Carlo Ancelloti lakini dakika ya 90′ na 91′ kinda Rodrygo alifunga mabao mawili ya haraka na kusawazisha mizani iliyopelekea mchezo kwenda dakika 30 za nyongeza ambao dakika ya 5 tu ilimtosha Karim Benzema kufunga kwa penati baada ya kuangushwa katika eneo la hatari.

Mpaka mchezo unamalizika City walikubali kichapo hicho cha 3-1 na kuwafanya Real Madrid kwenda Paris kuwavaa Liverpool wakiwa na kumbukumbu ya kuwafunga katika fainali kama hizo miaka kadhaa iliyopita.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala