Connect with us

Makala

Rc Tabora Aichongea Simba Sc

Mkuu wa mkoa wa Tabora Mh.Chacha Matiku ameahidi zawadi ya shilingi milioni 50 za kitanzania kwa wachezaji wa klabu ya Tabora United endapo watafanikiwa kuifunga Simba sc katika mchezo wa ligi kuu ya Nbc nchini unaotarajiwa kufanyika Novemba 28.

Ahadi hiyo imetolewa wakati wa tafrija fupi ya kiwapongeza mastaa wa klabu hiyo baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Yanga sc katika mchezo wa ligi kuu uliofanyika katika uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam.

Tabora United ilifanikiwa kuifunga Yanga Sc katika mchezo uliowashtua wengi na kuwafurahisha mashabiki wa simba sc kwa kuwa walifanikiwa kukaa kileleni mwa msimamo wa ligi kuu nchini.

Ushindi huo umeifanya timu hiyo kufikisha alama 17 katika michezo nane ya ligi kuu ya Nbc ikicheza michezo kumi na moja.

Mkuu huyo wa mkoa ameahidi endapo pia klabu hiyo itaifunga Simba sc katika mchezo wa ligi kuu utakaofanyika katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mkoani Tabora.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala