Connect with us

Makala

Prisons Yafurahia Ligi Kusimama

Kocha wa timu ya Tanzania Prisons,Mohammed Richard ‘Adolf’ amesema kiufundi kusimamishwa kwa michezo ligi kuu kumeifaidisha kikosi chake kwani atatumia muda huu kujipanga ili kumaliza vizuri michezo iliyosalia.

Amesema ushindi katika mechi zilizobaki utaiwezesha timu yake kumaliza katika nafasi za juu katika msimamo wa ligi kuu Tanzania Bara msimu wa mwaka huu 2019/2020 hii ni baada ya ligi kuu kusimamishwa Tanzania Bara ili kupambana na Virusi vya Corona vilivyoikumba Dunia.

Akizungumza Dar-es-salaam jana kwa njia ya simu ,Adolf alisema hana kikosi kikubwa na ndio maana wakati wa ligi ikiendelea wachezaji wake walishindwa kuendana na kasi  hivyo kusimama kwa ligi kuu kutaisadia sana timu yake kujiweka sawa na kufanya vizuri.

“Kwa kikosi kama cha kwangu dharura iliyotokea imekuwa na faida kubwa kwani sikuwa na kikosi kikubwa na mara nyingi nilikuwa nalalamika wachezaji wangu walikuwa wanachoka kiasi cha kupoteza muendelezo wa kupata ushindi kutokana na uchache wa wachezaji ila kwa kipindi hiki tutajipanga kwa michezo iliyobaki”alisema Adolf.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala