Connect with us

Makala

Pluijm Abwaga Manyanga Singida FG

Kocha Hans Van de Pluijm ameamua kuachia ngazi kuifundisha klabu ya Singida Fountain Gate kutokana na mfululizo wa matokeo yasiyoridhisha licha ya kuwa na kikosi kilichosheheni mastaa wa kila aina wenye uzoefu wa kutosha.

Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na klabu hiyo inaonyesha kwamba kocha huyo amejiudhuru ili kushughulikia matatizo yake binafsi huku klabu ikimshukuru kwa utumishi wake na kwa kipindi hiki timu hiyo itakua chini ya kocha msaidizi Mathias Lule.

“Kocha wetu Hans van der Pluijm hatutaendelea nae. Timu yetu itakuwa chini ya kocha Msaidizi Mathias Lule mpaka pale itakapoamuliwa vinginevyo”.Ilisomeka taarifa kutoka klabuni hapo.

Hans amekua na mchango mkubwa klabuni hapo akiisaidia timu hiyo kumaliza katika nafasi ya nne ya ligi kuu msimu uliopita huku pia akiivusha katika hatua inayofuatia ya kombe la shirikisho ambapo wamefanikiwa kuwatoa Jku ya Zanzibar kwa jumla ya mabao 4-3.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala