Connect with us

Makala

Phiri Aimaliza Nyasa Big Bullets

Mshambuliaji Moses Phiri amefanikiwa kufunga mabao matatu katika ushindi wa jumla wa mabao 4-0 dhidi ya Nyasa Big Bullets na kuiongoza Simba sc kufuzu hatua inayofuatia ya kichuano ya klabu bingwa barani Afrika ambapo sasa itakutana na miamba ya soka ya Angola ya 1 de Augosto.

Phiri awali katika mchezo wa kwanza aliifungia Simba sc goli la uongozi ugenini kabla ya John Boko kufunga bao la pili na kuwapa kazi ya ziada Nyasa ya kusawazisha katika uwanja wa Benjamini Mkapa ambapo napo wakakutana na kazi nzito ya kuikabili spidi ya Simba sc na kuambulia kipigo hicho cha mabaoa mawili yote yakifungwa na Phiri dakika za 30 na 51 na kuihakikishia klaby yake nafasi hatua inayofuatia.

Simba sc itaanzia ugenini dhidi ya miamba hiyo ya soka barani Afrika kati ya oktoba 7 na 14 ambapo watarudiana katika uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es salaam ana mshindi atajihakikisha kufuzu hatua ya makundi ya klabu bingwa ambapo atajipatia kitita cha takribani zaidi ya bilioni moja ya kitanzania.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala