Bodi ya ligi kuu nchini imetoa adhabu mbalimbali kwa wachezaji,viongozi na makocha wa ligi kuu pamoja na ligi daraja la kwanza na daraja la pili kutokana na makosa mbalimbali ya kinidhamu kutokana na kukiuka kanuni na sheria pamoja na miongozi ya soka nchini.
Adhabu hizo zimetokana na kikao cha kamati ya uendeshaji na usimamizi wa soka nchini kilichokaa Januari 27 ambapo katika kikao hicho kocha mkuu wa klabu ya Simba sc Pablo Franco amefungiwa mechi tatu pamoja na faini ya shilingi milioni tatu kwa ujumla kutokana na makosa ya kukataa kuongea na waandishi wa habari katika mechi dhidi ya Mbeya city,Mtibwa sugar na Kagera Sugar huku kosa la kupiga teke sanduku la kuhifadhia barafu akipewa adhabu ya kufungiwa mechi tatu.
Beki wa klabu ya Yanga sc Djuma Shabani nae amefungiwa jumla ya mechi tatu pamoja na faini ya kiasi cha shiligi milioni moja kwa kosa la kumpiga kiwiko mchezaji wa Polisi Tanzania katika mchezo ambao Yanga sc walishinda 1-0 huku pia tukio hilo likimponza mwamuzi Hans Mabena na wasaidizi wake waliopewa adhabu ya kuondolewa kuchezesha katika mizunguko mitatu ya ligi kuu.
Pia kamati hiyo imetoa onyo kali kwa Eng.Hersi Said,Azam Fc na Simba sc kwa kufanya makosa mbalimbali katika matukio tofauti tofauti kwemnye mechi za ligi kuu nchini.