Connect with us

Makala

Onana Aondoka Simba Sc

Klabu ya Simba Sc imetangaza kuachana na mshambuliaji Leandre Willy Esomba Onana baada ya kufikia makubaliano baina ya pande zote mbili kuachana kwa maslahi yao wote.

Onana aliyesajiliwa na Simba sc akitokea klabu ya Rayon Sports ya Rwanda ambapo aliibuka mfungaji bora msimu wa 2022/2023 na kuwavutia mabosi wa Simba Sc walioamua kuvunja benki kumsajili.

Msimu uliopita Onana hakua na msimu mzuri klabuni humo akishindwa kuwashawishi walimu Roberto Oliveira “Robertinho” na Abdelhack Benchika na kuishia kuwekwa benchi mara kwa mara.

Msimu huu Mwalimu Fadlu Davis ameridhia kuondoka kwa Onana ambaye anakwenda kujiunga na klabu Al Ahly Benghazi ya nchini Libya.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala