Connect with us

Makala

Okwi,Aucho Ndani ya The Cranes

Kiungo wa Yanga, Khalid Aucho na mshambuliaji Emmanuel Okwi ni miongo mwa wachezaji 30 walioitwa kwenye kikosi cha Timu ya Taifa ya Uganda kitakachoingia kambini hivi karibuni kwa ajili ya maandalizi ya kumenyana na Taifa Stars katika kuwania kufuzu michuano ya Afcon 2023.

Okwi mwenye umri wa miaka 30 kwa sasa ni mchezaji wa zamani wa Sc Club Villa,Simba sc na Yanga sc za nchini Tanzania aliondoka nchini mwaka 2019 na kujiunga na klabu ya Al Ittihad inayoshiriki ligi kuu nchini Misri ameitwa na kocha Milutin Sredojević maarufu kama “Micho” kama mshambuliaji huku kiungo wa Yanga sc Khalid Aucho akiitwa kama kiungo mwandamizi.

Aucho amekua na wakati mzuri tangu ajiunge na klabu ya Yanga sc akiwa na uhakika wa kucheza katika kikosi cha kwanza na kufanikiwa kushinda mataji kadhaa ya ligi kuu,ngao ya jamii na kombe la shirikisho la Azamsports huku hivi sasa akishiriki katika michuano ya kombe la shirikisho la Caf.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala