Connect with us

Makala

“Nina Ofa Tano Mezani”-Zahera

Kocha wa Yanga sc Mwinyi Zahera ameshangazwa na tetesi za kutimuliwa klabuni hapo zinazosambaa kwa kasi hivi sasa kufuatia matokeo yasiyoridhisha ya timu hiyo katika mechi za kirafiki na za hivi karibuni ikiwemo mechi ya klabu bingwa Afrika dhidi ya Township Rollers.

Kocha huyo amesema jambo hilo linamkosesha utulivu katika kuiandaa timu inayokabiliwa na mchezo mgumu wa kimataifa dhidi ya Rollers ugenini nchini Botswana.

“Nina ofa tano mezani hata nikiondoka Yanga nitachagua  wapi nitaelekea,kuna timu za Ufaransa,kongo na Nigeria zote zinanihitaji”.

Kocha huyo aliyejiunga na Yanga msimu uliopita alikua na wakati mgumu ambapo alikuta kikosi ambacho hakijitoshelezi pia hali ya uchumi haikua njema klabuni hapo tofauti na msimu huu ambapo timu imefanya usajili wa kutosha hivyo mashabiki wanategemea makubwa kutoka kwake.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala