Connect with us

Makala

Kumenoga Kmc,M-bet Washusha Neema

Timu ya manispaa ya kinondoni (Kmc) imeingia udhamini mnono wenye thamani ya Bilioni moja na kampuni ya kubashiri ya M-bet baada ya kusaini mkataba wa miaka mitano.

Akiongea na waandishi wa habari wakati wa hafla ya kutia saini makubaliano hayo meya wa manispaa hiyo Benjamini Sitta alisema mkataba huo utakua unaboreshwa kila mara ikiwemo kuongeza bonasi na kusaidia ujenzi wa uwanja mpya wa klabu hiyo.

Naye afisa masoko wa M-bet amesema wamesukumwa kuidhamini timu hiyo baada ya kuwa na uongozi imara “tumeamua kuidhamini timu hii baada ya kuona¬† timu inaongozwa kiuweledi huku kukiwa na mipango ya muda mrefu na muda mfupi.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

More in Makala