Connect with us

Makala

Ni Ufaransa Vs Argentina Wc 2022

Fainali ya kombe la dunia sasa ni dhahiri ni Ufaransa dhidi ya Argentina baada ya jana Ufaransa kufanikiwa kumfunga Morocco mabao 2-0 katika mchezo wa nusu fainali ya pili baada ya juzi Argentina kumfunga Crotia na timu zote mbili sasa zitakutana katika mchezo wa fainali siku ya Jumapili.

Ikianza na mshambuliaji mmoja halisi Oliver Giroud ambaye alisaidiwa na Kylian Mbappe na Antoine Griezman na Osmane Dembele Ufaransa ilipata bao la mapema dakika ya tano likifungwa na Theo Hernandez baada ya mabeki wa Morroco kushindwa kuondoa mpira uliopigwa na Mbappe na kumkuta mfungaji.

Kuumia kwa nahodha wa Morroco beki R.Sais kuliongeza pigo ambapo walilazimika kucheza na mfumo wa mabeki wanne huku wakishambulia kwa kasi na krosi ambazo nyingi ziliokolewa na Rafael Varane na Konate huku eneo la Kiungo kukiwa na vita kali kati ya Fofana na Amrabat.

Mshambuliaji wa Eintracht Frankfurt ya Ujerumani Randal Kolo Muani aliimaliza mechi dakika ya 79 baada ya kufunga bao la pili ambalo lilihitimisha rasmi safari ya Morocco katika michuano hiyo huku wakiweka rekodi ya kuwa timu ya kwanza kutoka Afrika kufuzu hatua ya nusu fainali.

“Tuliifunga timu ngumu ya Ubelgiji, tukaifunga timu ngumu zaidi ya Ureno, na tukaishinda Hispania ambayo imewahi kuwa mabingwa wa dunia. Tulipokua 11 uwanjani na wao 11 tuliwashinda. Tulipokua 10 na wao 11 bado tuliwazidi nguvu. Haikua rahisi lakini dunia imepata ujumbe kuwa soka la Afrika si la kubeza. Tumesogea hatua moja zaidi ya waliposogea ndugu zetu wa Senegal (2002) na Ghana (2010). Tunaweza kusogea hatua kubwa zaidi kama nchi zote za Afrika zitafanya uwekezaji zaidi katika soka” Maneno ya Walid Regragui baada ya mchezo huo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala