Connect with us

Makala

Neymar Aanza Visa Uarabuni

Mshambuliaji wa Al Hilal Neymar Jr hana tena furaha huko Saudia Arabia hii ni baada ya kuwa na mzozano na kocha wake Jorge Jesus kwenye mechi dhidi ya Navbahor  katika michuano ya kombe la mabingwa AFC wiki iliyoisha.

Kocha huyo alimkosoa Neymar jambo ambalo Neymar Jr alichukizwa kisha kumjibu vibaya na inasemekana Neymar Jr ameuambia uongozi wa Al Hilal kama wanataka yeye aendelee kubakia Saudia wamfute kazi kocha huyo Jorge Jesus.

Katika mchezo huo Al Hilal fc walilazimika kusawazisha dakika za mwisho baada ya wageni Navibahor kutangulia kupata bao dakika ya 52 ya mchezo likifungwa na Toma Tabatabze ndipo baada ya mchezo huo kocha Jorge Jesus akatoa kauli hiyo.

Kutokana na matokeo hayo kikosi cha timu hiyo sasa kipo nafasi ya tatu ya msimamo kikiwa na alama moja tu katika kundi D la michuano hiyo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala