Mshambuliaji wa klabu ya Yanga sc Clement Mzize amepata ofa nono ya kujiunga na klabu ya Zamaleck Fc ya nchini Misri kujiunga na klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu.
Ofa ya Zamalek Fc kwenye usajili wa Clement Mzize kutoka Yanga sc ni Bilioni 2.6 lakini Zamalek wanataka kulipa kwa awamu mbili dau hilo.
Kwa mujibu wa ofa hiyo awamu ya kwanza watatoa Bilioni 2 na awamu ya pili watatoa milion mia sita (6) iwapo watatwaa Ubingwa kitu ambacho mabosi wa klabu hiyo wamegoma wakihitaji walipwe pesa hiyo mara moja.
Mpaka sasa bado mazungumzo baina ya mabosi wa klabu hizo yanaendelea vizuri ambapo pia mchezaji huyo ametengewa dau nono la usajili na mshahara mzuri.
Pamoja na ofa ya Zamaleck Fc pia Yanga sc ina ofa kutoka Wydad Athletic Club na Al Ittihad ya Libya ambao nao wametuma ofa moja kwa moja.