Connect with us

Soka

Guardiola Alia na VAR

Kocha wa manchester city Pep Guardiola amelalamika kitendo cha mwamuzi wa video(Var) kumnyima penati mbili wakati akipokea kipigo cha mabao 3-1 dhidi ya Liverpool katika uwanja wa Anfield na kuweka matatani nafasi ya kutwaa ubingwa msimu huu.

Man city walilamikia tukio la dakika za awali wakati ilipodhaniwa beki Trent Alexander-Arnord ameunawa mpira kabla ya Fabinho kumtungua kipa Claudio Bravo dakika ya 6 na kufanya vijana wa Guardiola kuchanganyikiwa ambapo dakika saba baadae waliruhusu goli la pili likifungwa na Mohamed Salah akimalizia krosi ya Robertson.

Liva walijihakikishia pointi zote tatu kabla ya kipindi cha pili kwa makosa ya kipa Claudio Bravo yaliyompa goli Sadio Manne baada ya kushindwa kuokoa kichwa cha kuchumpa.

Ushindi huo unafanya Liver kuwa na alama nane zaidi ya Man city huku wakiwa wameshinda michezo 11 katika ya 12 msimu huu na kutoa matumaini ya kutwaa ubingwa walioukosa kwa miaka 30.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Soka