Beki wa kati wa Simba Sc Abdulrazack Hamza (22) amefanya mazoezi na wachezaji wenzake kwaajili ya mechi ya pili ya Fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya RS Berkane utakaofanyika siku ya Jumapili Mei 25 2025 katika uwanja wa Amaani Visiwani Zanzibar.
Hamza Baada ya kushindwa kumaliza mechi ya Fainali ya kwanza pale Morocco, sasa yupo tayari kwaajili ya mechi ya pili ambapo amefanikiwa kushiriki mazoezi na wenzake akiwa fiti kabisa.
Sasa kocha Fadlu Davis atakua na wigo mpana wa kuchagua kati ya Hamza na Che Malone Fondoh pamoja na Chamou Karabou kuona nani anaweza kuanza katika mabeki wawili wa kati.
Simba sc itakua na wakati mgumu ikitafuta kupindua meza baada ya kuruhusu mabao 2-0 katika mchezo wa kwanza uliofanyika nchini Morocco.