Connect with us

Makala

Mwanuke Awagomea Mabosi Simba sc

Winga Jimmyson Mwinuke amegoma kutolewa kwa mkopo na uongozi wa klabu hiyo kwenda klabu nyingine akishinikiza abaki kikosini ama wavunje mkataba kwa makaubaliano ya pande mbili ili akatafute maisha katika klabu zingine.

Winga huyo ni mmoja katika ya wachezaji ambao uongozi wa klabu hiyo upo mbioni kuwatoa kwa mkopo ili wakaboreshe viwango vyao baada ya kushindwa kumvutia mwalimu Roberto Oliveira “Robertinho”.

Bado haijafahamika sasa kutokana na winga huyo kugoma pendekezo hilo la awali la uongozi juu ya hatma yake klabuni hapo kama watakubali kumuacha moja kwa moja ama ataendelea kubaki kikosini.

Mwanuke alisajili na Simba sc misimu mitatu iliyopita akitokea klabu ya Gwambina Fc iliyokua na makazi yake kanda ya ziwa lakini tangu atue klabuni hapo amekua na nafasi finyu ya kucheza.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala