Connect with us

Makala

Mwamposa Kuishuhudia Simba Sc Vs Al Masry

Klabu ya Simba Sc imemualika Mtume Bonifasi Mwamposa kuwa moja ya wageni rasmi katika mchezo wa kombe la shirikisho dhidi ya Al Masry utakaofanyika April 9 2025 katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Mwaposa moja ya Viongozi wa dini wenye ushawishi mkubwa nchini ataungana na mkuu wa mkoa wa Tabora Mh.Paul Chacha kuwa moja ya wageni waalikwa kuelekea mchezo huo wa kukata na shoka ambao Simba sc inapaswa kushinda kuanzia mabao matatu.

Akizungumza wakati akiwa katika Uzinduzi wa hamasa katika maeneo mbalimbali nchini meneja wa Idara ya habari na mawasiliano wa Klabu ya Simba Sc Ahmed Ally amesema kuwa lengo la kumualika Mwamposa ni kuondoa Mashetani katika mchezo huo kwa maana pia kuna watu hawairakii mema klabu hiyo.

“Safari hii tumedhamiria Ubaya Ubwela na tunamualika kila mtu mwenye mchango mkubwa kwenye jamii hii, wacahwi wengi ndugu zangu, kuna watu wamekunja nafsi kwelikweli. Kwa mantiki hiyo namtangaza mgeni mwingine maalumu Mtume Boniface Mwamposa (Buldoza). Tunafanya mazungumzo naye pia ikiwezekana kesho tukawauzie waumini wake tiketi”,Alisema Semaji Ahmed Ally akiongea na Wanasimba wa Ukonga Mazizini.

Pia kutokana na sakata la hivyo karibuni la mkuu wa mkoa wa Tabora Mh.Paul Chacha dhidi ya Klabu ya Yanga sc,Klabu hiyo imeamua kumualika katika mlengo wa kudumisha utani wa jadi baina yao na kuongeza hamasa.

“Tunafanya utaratibu wa kumwalika Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Paul Chacha aje kujumuika na Watanzania wenzake kuangalia mwakilishi wa nchi akienda nusu fainali. Tunamwalika sababu ya mchango wake wa kuhamasiha michezo na ajifunze namna maandalizi ya kimataifa yanafanyika kwa ajili ya kuiandaa timu yake ya Tabora United.”Alisema Ahmed Ally.

Simba sc baada ya kuruhusu bao 2-0 dhidi ya Al Masry nchini Misri sass inapaswa kulipiza kisasi katika mchezo ujao ambao unatarajiwa kufanyika April 9 2025 na tayari tiketi zimeanza kuuzwa ambapo ya gharama ya chini ni Tsh 5000/=.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala