Connect with us

Makala

Mwali wa AFL Atambulishwa Rasmi Dar

Rais wa Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) Patrice Motsepe amelitambulisha rasmi Kombe ambalo atakabidhiwa Bingwa wa michuano ya African Football League (AFL) ambalo litaanza kugombaniwa hivi leo jijini Dar es salaam.

Motsepe amelitambulisha kombe hilo mbele ya waandishi wa habari katika mkutano uliofanyika jijini Dar es salaam mchana wa leo katika hoteli ya Hyatt Regency ambapo pia wageni muhimu walihudhuria akiwemo kocha Arsenal Wenger na Dk.Damas Ndumbaro ambaye ni Waziri wa Sanaa,Utamaduni na Michezo.

Katika mazungumzo yake Motsepe alisema kuwa mwakani wanatarajia michuano hiyo kushirikisha jumla ya timu 24 ambazo zitachaguliwa kutokana na ranki za Caf na ligi kuu za nyumbani.

“Msimu ujao tutakuwa na timu 24 kwenye michuano ya African Football League tutazipata kupitia ranki za CAF pamoja na mafanikio yake katika ligi za nyumbani,” Alisema Rais wa CAF, Patrice Motsepe.

“Nawashukuru viongozi wa timu zote nane zinazoshiriki michuano ya African Football League pamoja na zile 24 ambazo zitashiriki mwakani.”Alimalizia kwa kusema Rais huyo wa Caf ambaye ni raia wa nchini ya Afrika ya kusini.

Katika ufunguzi wa michuano hiyo jioni ya leo Simba sc itavaana na Al Ahly katika mchezo wa kukata na shoka ambapo mshindi wa mechi mbili za nyumbani na ugenini atakata tiketi ya kuingia nusu fainali.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala