Connect with us

Makala

Mwakinyo Asota Rumande

Jeshi la polisi mkoani Tanga limeendelea kumshikiria Bondia Hassan Mwakinyo kwa kosa la kumpiga na kumjeruhi mkazi wa mkoani humo Mussa Ally kwa kosa la kumtuhumu kuwa ni mwizi baada ya mtuhumiwa huyo kuingia nyumbani kwa bondia huyo bila taarifa.

Akizungumza na waandishi wa Habari mapema hivi leo kamanda wa polisi mkoani humo Almachius Mchunguzi amesema kuwa bondia huyo anashikiliwa kwa kosa la kumjeruhi mkazi huyo ambaye ni mvuvi mwenyeji wa mkoa huo.

Kamanda huyo amesema uchunguzi utakapokamilika atatoa taarifa kwa vyombo vya habari ikiwa ni sambamba na kumfikisha mahakamani ili ajibu tuhuma zitakazomkabili katika kosa hilo.

Amesema wamemkamata kwa tuhuma za kumjeruhi mvuvi, ambapo ni tuhuma za jinai mtu yeyote akifanya makosa kama hayo bila kuangalia nafasi yake kwenye jamii, anatakuwa kuchukuliwa hatua za kisheria na suala la umaarufu haliwezi kubadili kile kilichotendeka.

“Jeshi la polisi Mkoa wa Tanga linamshikilia Hassan Mwakinyo (29) mkazi wa Sahare jijini Tanga kwa kumshambulia na kumjeruhi Mussa Ally mkazi wa eneo hilo ambae ni mvuvi,uchunguzi wa tukio hili unaendelea na ukikamilika mtuhumiwa atapelekwa mahakamani,” amesema Mchunguzi.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala