Connect with us

Makala

Mwakinyo Afafanua Kufungiwa

Bondia Hassan Mwakinyo amefafanua kuhusu kufungiwa kwake na shirikisho la ngumi nchini Uingereza kucheza mapambano ya ngumi nchini humo kwa kipindi cha siku arobaini na tano baada ya pambano lake na Ian Smith ambalo alipigwa kwa Tko raundi ya nne pambano lililofanyika jijini Liverpool nchini humo.

Habari hiyo ambayo iliripotiwa na  mtandao wa ngumi duniani uitwao Boxrec kuwa Mwakinyo amefungiwa kushiriki mapambano hayo nchini humo na kuzua taharuki miongoni mwa wadau wa ngumi nchini wakiwemo waandishi wa habari huku sababu za kufungiwa zikiwa hazijulikani lakini habari njema ni kwamba kufungiwa huko kucheza mapambano ya ngumi kwa mujibu wa sheria za ngumi duniani ni kwamba kifungo hicho ni kwa ajili ya nchi ya Uingereza pekee na si nchi zingine.

Kama haitoshi Bondia huyo wa kwanza kwa ubora nchini katika uzani wa kati na wa pili barani Afrika ametolea ufafanuzi kuwa amefungiwa kwa siku 45 pekee na hiyo inatokana na kupigwa kwa Tko katika pambano lake lililopita nchini humo hivyo anatakiwa kutekeleza kifungo hicho kama zilivyo sheria na taratibu za nchi hiyo ya Uingereza ambapo bondia akipigwa kwa Tko analazimika kutopigana kwa muda ili kupata nafuu na kurudisha mwili kutoka katika majeraha.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala