Connect with us

Makala

Mukoko Atua Tp Mazembe

Kiungo Mukoko Tonombe ameachana na klabu ya Yanga sc na kutua klabu ya Tp Mazembe ya nyumbani kwao nchini Congo kwa mkataba wa miaka miwili baada ya dili hilo kuwa na sintofahamu kwa muda wa wiki kadhaa.

Awali ilidaiwa kwamba kiungo huyo ataenda Tp mazembe kwa mabadilishano na winga Chico Ushindi lakini mchezaji huyo aligoma kwa maana hakufahamu iwapo anakwenda kwa mkopo ama anasajiliwa moja kwa moja huku pia sababu za maslahi zikitajwa na kulazimika mabosi wakubwa wa jangwani kuingilia kati na kumtuliza hadi hapo ilipotangazwa rasmi na klabu hizo kuhusu kukamilika kwa usajili huo.

Mukoko Tonombe ni moja ya nguzo muhimu katika eneo la kiungo la klabu ya Yanga sc tangu kusajiliwa kwake huku akiweza kupata tuzo ya mchezaji bora wa klabu hiyo kwa msimu uliopita.

Kuondoka kwa Mukoko Yanga sc kumechangiwa kwa kiasi kikubwa na kukosa nafasi katika kikosi cha kwanza hali iliyosababishwa na mfumo wa mwalimu Nabi kuwapendelea zaidi umoja wa Yanick Bangala na Khalid Aucho huku sheria ya kutumia wachezaji nane wa kigeni nayo ikichangia staa huyo kukaa jukwaani mara kwa mara.

Yanga sc ilionyesha nia ya kumuongezea mkataba kiungo huyo wa shoka lakini mahitaji yake ya kuhakikishiwa nafasi ya kucheza mara kwa mara yalikuwa magumu kuyatekeleza kwa mwalimu Nasredine Nabi hali iliwalazimu Yanga sc kumuuza staa huyo ili asiondoke bure mwishoni mwa msimu.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala