Connect with us

Makala

Mugalu,Inonga Waingia Caf

Mshambuliaji Chris Mugalu na beki Henock Inonga pamoja na winga Benard Morrison wameingia katika orodha wa wachezaji bora wa wiki katika michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika.

Iko hivi kila baada ya michezo ya kombe la shirikisho hatua ya makundi Caf hutangaza kikosi bora cha wiki ambapo kutokana na kufanya vizuri katika mchezo dhidi ya Us Gendamarie wachezaji hao wameingia katika kikosi bora ambapo Mugalu amewekwa kama mshambuliaji wa kati huku Inonga akiwekwa beki ya kati na Morrison akiwekwa nafasi ya winga wakiungana na wachezaji kutoka timu zingine kutengeneza kikosi hicho bora cha Caf.

Simba sc imefanikiwa kuingia hatua ya robo fainali ikiungana na Rs Berkanehuku Al Ahly Tripoli ya Libya na Pyramids ya Misri hizi zilikuwa kundi A na Orlando Pirates ya Afrika Kusini na A Ittihad ya Libya kutoka kundi B.

TP Mazembe ya DR Congo na Al Masry ya Misri kutoka kundi C ambapo kesho Jumanne inatarajiwa kuchezwa droo ya mechi za robo fainali na Simba inaweza kukutana na Al Ahly Tripoli, Orlando Pirates au TP Mazembe ambazo zimemaliza vinara katika makundi yao.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala