Connect with us

Makala

Mudathir,Aggrey Wahitajika Simba sc

Wachezaji Mudathir Yahaya na Aggrey Morris waliosimamishwa na klabu ya Azam Fc wapo mbioni kujiunga na klabu ya Simba sc iliyoonesha nia ya kuwasaini wote wawili pindi mazungumzo yatakapokamilika.

Wachezaji hao wameichezea Azam Fc na timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa stars) kwa mafanikio makubwa kwa nyakati tofautitofauti huku pia wakiwa na mchango mkubwa klabuni Chamazi yalipo makao makuu ya Azam Fc.

Kusimamishwa kwa muda usiojulikana inatajwa kuwa ni sababu ya wachezaji hao kuhitaji kuondoka klabuni hapo pamoja na kutuhumiwa kuwa watovu wa nidhamu na uongozi wa klabu hiyo.

Simba sc inatajwa kuhitaji saini ya kiungo mmoja mzawa mwenye uwezo wa kushambulia na kuzuia kwa pamoja huku pia ikihitaji beki mbadala wa Serge Pascal Wawa ambaye amekalia kuti kavu pamoja na wachezaji kadhaa wa kimataifa akiwemo winga mshambuliaji Moses Phiri pamoja pia ikimhitaji Cletous Chama arejee baada ya kuonyesha nia ya kurudi huku pia ikitajwa Emmanuel Okwi naye akihitaji kurudi klabuni hapo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala