Connect with us

Makala

Mudathir Atua Yanga sc,Akiwasha Mapinduzi Balaa

Kiungo wa zamani wa klabu ya Azam fc Mudathir Yahya Abass amejiunga na klabu ya Yanga sc kwa mkataba wa miaka miwili akiwa kama mchezaji huru baada ya kuachana na Azam Fc katika dirisha kubwa la usajili la mwanzoni mwa msimu huu.

Baada ya kukaa takribani miaka mitano akiwa huru hatimaye kiungo huyo anatambulishwa katika kikosi cha Yanga sc na moja kwa moja baada ya utambulisho staa huyo aliekea Zanzibar kujiunga na kambi ya timu hiyo kujiandaa na michuano ya kombe la Mapinduzi ambapo Yanga sc imemenyana na KmKm na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa 1-0 huku Mudathir akionyesha kiwango kizuri licha ya kucheza takribani dakika 20 za mwisho.

Yanga sc sasa itacheza mchezo wa mwisho dhidi ya Singida Big Stars ambayo ilimfunga Kmkm mabao 2-0 ambapo mshindi atafuzu kwenda nusu fainali ya michuano hiyo ama sare ya magoli yeyote basi Singida Big stars atafuzu hatua inayofuata.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala