Connect with us

Makala

Mudathir Atia Fora Caf

Kiungo wa klabu ya Yanga sc Mudathir Yahya Abass ametia fora katika michuano ya kimataifa ikiwa ni msimu wake wa kwanza tangu ajiunge na Yanga sc baada ya bao lake alilolifunga dhidi ya Tp Mazembe kufanikiwa kuchaguliwa kuwa goli bora katika michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika.

Iko hivi,baada ya kumalizika kwa mechi za hatua ya makundi shirikisho la soka barani Afrika (Caf) huchagua goli bora katika hatua hiyo ambapo mshindi ni yule atakayepata kura nyingi za mashabiki kupitia mitandao ya kijamii ya shirikisho hilo ambapo katika orodha ya mabao hayo alikua akishindana na Aymen Mahious alyepata kura 20.8%,Aubin Kramo Kouamé aliyepata kura 5.2% Mudathiri Yahya aliyepata kura 70.5% na Paul Acquah.

Kura hizo huamuliwa na mashabiki ambao hupiga kura katika mitandao ya Caf kisha shirikisho hutaja mshindi kwa kuhesabu kura hizo hivyo bao alilofungwa Mudathir katika ushindi wa 3-1 dhidi ya Tp Mazembe ndio bao bora katika hatua ya makundi ya kombe la shirikisho barani Afrika.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala