Connect with us

Makala

Morroco,Senegal Watinga Robo Fainali Afcon

Timu ya Taifa ya Morroco imefanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya michuano ya Afcon 2021 baada ya kuifunga timu ya Malawi kwa 2-1 katika mchezo mkali na wa kusisimua uliofanyika katika uwanja wa Ahmadou Ahidjo Jijini Yaoundé nchini Cameroon.

Malawi walikua wa kwanza kuwashangaza mashabiki baada ya kupata goli la mapema dakika ya saba kupitia kwa Hellings Frank Mhango mshambuliaji wa Orlando Pirates ya Afrika Kusini lakini kuingia kwa bao hilo kuliwachokoza Morroco ambao walishambulia lango la Malawi mpaka walipopata bao la kusawazisha kupitia kwa mshambuliaji wa Sevilla ya Hispania, Youssef En-Nesyri  dakika ya 47 na beki wa Paris-Saint Germain, Achraf Hakimi Mouh kufunga la ushindi dakika ya 70 lilohakikisha kuwapeleka Robo Fainali Simba wa Atlasi.

Kwa ushindi huo Morocco itakutana na mshindi kati ya Ivory Coast na Misri na Senegal itakutana na mshindi kati ya Mali na Equatorial Guinea zinazokamilisha Hatua ya 16 Bora kesho.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala