Connect with us

Makala

Morisson aishida Yanga CAS

Mahakama ya usuluhishi wa michezo duniani(CAS) imetupilia mbali rufaa ya kesi ya kimkataba kati ya klabu ya Yanga na mchezaji wa klabu ya Simba Benard Morisson katika hukumu iliyotoka hii leo.

Yanga waliamua kukata rufaa CAS baada ya kutoridhishwa na maamuzi ya kamati ya sheria na hadhi za wachezaji mwaka 202o ambapo pia Morisson alishinda.

Klabu hiyo ilikua inataka kurudishiwa zaidi ya milioni 460 za usajili na mchezaji huyo kwa kile walichodai kuwa mchezaji huyo amekiuka mkataba kwa kusaini Simba huku akiwa bado ana mkataba na Yanga.

CAS imeiamuru klabu ya Yanga kulipa Tsh milioni 12 kama gharama za uendeshaji wa kesi hiyo.

Makamu mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela amesema kuwa wamkubali hukumu hiyo ya CAS kwa kusema imetokana na ushahidi wao kuonekana una mapungufu.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala