Connect with us

Makala

Moloko,Sure Boy kuwakosa Bamako

Wachezaji Jesus Moloko na Salum Abubakar wataukosa mchezo wa leo dhidi ya Real Bamako ya nchini Mali utakaofanyika katika uwanja wa Benjamini Mkapa kutokana na sababu mbalimbali kwa mujibu wa kocha wa timu hiyo Nasredine Nabi.

Kocha huyo alisema kuwa Sure Boy amefiwa na mtoto wake wa kiume aitwaye Feisal Salum Abubakari ambaye tayari amezikwa jana jioni huku Jesus Moloko akisumbuliwa na maumivu ya mguu baada ya kuumia katika mchezo dhidi ya Tanzania Prisons ambao ulifanyika katika uwanja wa Chamazi Complex na Yanga sc kuibuka na ushindi wa mabao 4-1.

“Moloko bado hajawa imara ripoti yake ya mazoezi ya mwisho itaamua kama ataanza kikosi cha kwanza ama la lakini ukweli ni kuwa alipata maumivu.

“Wengine ni wale wenye matatizo ya kifamilia lakini tupo tayari kupambana kupata matokeo,”.Alisema Nabi ambaye taarifa zinasema kwamba tayari ana ofa kadhaa za baadhi ya timu kubwa barani Afrika ikiwemo Tp Mazembe ya nchini Congo Drc.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala