Connect with us

Makala

Moalin ama Mgunda Kutua Coastal

Kabu ya Coastal Union inaangalia uwezekano wa kumchukua mmoja kati ya Juma Mgunda ama Abdihamid Moalin kuja kuwa kocha mkuu wa klabu hiyo baada ya kuachana na benchi lake la ufundi hivi karibuni.

Klabu hiyo awali iliangalia uwezekano wa kumpata Moalin kocha wa zamani wa Azam Fc ambapo mazungumzo yalifanyika japo hayajafikia hatua nzuri zaidi huku pia wakifuatilia mwenendo wa Juma Mgunda katika klabu ya Simba sc ambapo taarifa zinadai kuwa anaweza kuhamishiwa Simba queens.

Mgunda mpaka sasa ni kocha msaidizi wa timu kubwa lakini kuna uwezekano wa kuhamishiwa Simba queens baada ya kocha Roberto Oliveira kutaka kuja na wasaidizi wake mwenyewe.

Endapo suala hilo litafanikiwa basi Coastal itaingia katika mbio za kumshawishi kocha  huyo ajiunge na timu hiyo kama kocha mkuu ambapo hapo awali aliitumikia klabu hiyo na kutengeneza kikosi hatari kilichoingia fainali ya kombe la shirikisho la Azam ambapo walikosa ubingwa kwa mikwaju ya penati baada ya kutoka 3-3 katika dakika 90.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala