Connect with us

Makala

Mo Amteua Tena Magori

Bosi wa klabu ya Simba sc Mohamed Dewji amemteua Crescentius Magori kuwa mshauri wake mkuu baada ya kuridhishwa na kazi yake aliyoifanya kwa mara ya kwanza tangu ameteue katika cheo hicho klabuni hapo miaka michache iliyopita.

Magori kufuatia uteuzi huo kama mshauri mkuu wa bosi huyo katika masuala ya uendeshaji wa klabu hiyo anaungana na Salum Abdalah aliteuliwa kuwa mwenyekiti wa klabu hiyo akimuwakilisha muwekezaji huku Murtaza Mangungu akiwa mwenyekiti upande wa wanachama wa klabu hiyo.

“Kufuatia kazi nzuri aliyoifanya Ndugu Crescentius Magori katika kunishauri kuhusu maendeleo ya Klabu yetu ya Simba, nimeteua tena kwa kipindi kingine kuwa Mshauri wangu kuhusu michezo kwa ujumla na maendeleo ya Klabu yetu ya Simba. Hongera Ndugu Magori!”ilisomeka ujumbe wa bosi huyo katika mtandao wa instagram.

Bosi huyo anatajwa kuwa turufu ya ushindi kwa muwekezaji huyo mwenye hisa asilimia 49 klabuni hapo kwani ana uzoefu wa kutosha pamoja na kufahamu fitna za soka la kisasa barani Afrika.

 

 

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala