Connect with us

Makala

“Mnahesabu Lakini”

Klabu ya soka ya Simba sc sasa rasmi imeanza kurejesha heshima yake iliyopotea kwa takribani misimu miwili baada ya kufanikiwa kutwaa taji la kwanza msimu huu la ngao ya jamii baada ya kuwafunga Yanga sc kwa penati 3-1 katika mchezo wa fainali uliofanyika katika uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga sc.

Simba sc iliingia fainali ya michuno hiyo baada ya kuwafunga Singida Fountain Gate Fc katika hatua ya nusu fainali huku Yanga sc ikifunga 2-0 Azam Fc katika mchezo wa hatua hiyo ya nusu fainali ya kukutana fainali na Simba sc iliyowazidi maarifa ya upigaji penati na hatimaye kutwaa taji hilo la kwanza.

Yanga sc ilitawala mchezo kwa takribani dakika zote tisini huku ikikosa magoli kutokana na kuwa na safu butu ya ushambuliaji iliyokua ikiongozwa na Clement Mzize na Kennedy Musonda ambao licha ya kupewa huduma ya kutosha na viungo wa ushambuliaji wakiongozwa na Khalid Aucho na Maxi Nzengeli.

Uwepo wa Chama,Luis Miqquisone na Saido Ntibanzokiza katika eneo la kiungo la Simba sc lilileta uzito wakati wa kufanya mashambulizi kutokana na kukosa spidi upande wa winga zote mbili na kutegemea kushambulia kupitia eneo la katikati mwa uwanja pekee eneo ambalo lilikua gumu kupitika kutokana na uimara wa walinzi wa Yanga sc Bakari Mwamnyeto na Ibrahim Hamad.

Mwamuzi Jonesia Lukyaa hakua na jinsi zaidi ya kuamuru matuta baada ya suluhu dakika tisini za mchezo ambapo kipa Ally Salim aliibuka shujaa akicheza penati tatu za Yanga sc akianza na iliyopigwa na Khalid Aucho,Pacome Zouzou na Yao Kuoasi huku upande wa Simba sc Saido Ntibanzokiza na Moses Phiri walikosa huku Andre Onana,Jean Baleke na Mzamiru Yassin wakipata penati zao na kuipa Simba sc taji la kwanza msimu huu.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala