Connect with us

Makala

Mkude Kuikosa Berkane

Kiungo wa klabu ya Simba sc Jonas Mkude anatarajiwa kuikosa mechi dhidi ya Rs Berkane ya nchini Morroco katika mchezo wa tatu wa timu hiyo utakaofanyika leo usiku nchini Morroco ikiwa ni mchezo wa tatu wa klabu hiyo katika kundi D.

Hii ni mechi ya pili mfululizo kwa mkude kuikosa kutokana na kusumbuliwa na majeraha akiwa tayari amezikosa timu za Us Gendamirie katika sare ya moja moja ugenini na sasa atalazimika kuikosa Berkane.

Simba sc tayari ipo nchini Morroco ikitetea nafasi yake ya uongozi wa kundi D baada ya kuichapa Asec Mimosa na kutoa sare ugenini na Gendamarie na kushika uongozi wa kundi na sasa wana kibarua cha kuhakikisha wanapata alama tatu ugenini.

Kutokana na kutokuwepo kwa mkude Simba sc inaweza kuwatumia Erasto Nyoni,Mzamiru Yassin ama Thadeo Lwanga ambaye amerejea kutoka majeraha kucheza sambaba na Saido Kanoute katika eneo la kiungo wa ulinzi.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala