Connect with us

Makala

Mkali Wa Kucheka Na Nyavu Atua Yanga

Mshambuliaji namba moja wa klabu ya Mbao FC, Waziri Junior leo Agosti 2, ametambulishwa rasmi kuwa mali ya Yanga baada ya kusaini dili la miaka miwili akiwa ni mchezaji huru baada ya mkataba wake wa mwaka mmoja kukamilika.

Junior amecheka na nyavu ndani ya ligi kuu bara kwa msimu wa 2019/20 akifunga jumla ya mabao 12 akiwa ni namba moja ndani ya kikosi hicho.

Mchezo wa mwisho kuvaa jezi ya Mbao FC ilikuwa jana, Agosti Mosi, mbele ya Ihefu kwenye mchezo wa playoff uliochezwa Uwanja wa Kirumba ambapo alifunga mabao mawili.

Huu unakuwa ni usajili wa nne kwa Yanga msimu huu ilianza na Zawad Mauya kutoka Kagera Sugar ikafuata kwa Bakari Mwamnyeto kutoka Coastal Union na Yassini  Mustapha wa Polisi Tanzania.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala