Connect with us

Makala

Miquissone Bado Kidogo

Usajili uliosubiriwa kwa hamu na mashabikiwa klabu ya Simba sc Luis Miqqueson hatimaye jana aliingia katika mchezo wa Simba sc Day dhidi ya Power Dynamos ya Zambia na kufanikiwa kuwaonyesha makali yake ambayo mashabiki waliyakumbuka tangu aondoke klabuni hapo.

Lakini tofauti na matarajio ya wengi bado mchezaji huyo hajawa Fiti ya kutosha kuweza kupambana kutokana na kutocheza kwa muda mrefu alipokua katika klabu ya Al-Ahly licha ya kutolewa kwa mkopo mara kadhaa.

Mchezaji huyo jana alionekana kuwa akili ya mchezo bado ipo pamoja na maarifa ya kutosha lakini tatizo lilikua katika umiliki wa mpira pamoja na nguvu za kupambana zilikua zipo chini kutokana na kutocheza mara kwa mara.

Kocha wa viungo wa klabu ya Simba sc ana kazi nzito ya kurejesha fitnes ya mchezaji huyo ambaye pia jana alikua ana jicho la pasi lakini alikata upepo mapema sana tofauti na matarajio ya wengi.

Pia kocha Robertinho kwa kikosi alichonacho sasa inabidi mastaa wapambane kupata nafasi ya kuanza kikosi cha kwanza cha klabu hiyo kutokana na kila namba kuwa na wachezaji wawili ama zaidi.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala