Connect with us

Makala

Miqqueison Arejea Simba sc

Ni kama imebaki utambulisho tu baada ya kiungo mshambuliaji wa klabu ya Al Ahly Fc ya nchini Misri Luis Miqquisson kufanikiwa kuvunja mkataba wake uliokua umesalia wa miaka miwili na klabu hiyo.

Awali Simba sc ilikua na nia ya kumsajili staa huyo lakini walipoulizia gharama zake za usafiri ambazo zilifikia kiasi cha dola laki tatu ambazo ni zaidi ya shilingi milioni mia saba walirudi nyuma na kumuomba mchezaji mwenyewe kupambana kuvunja mkataba huo jambo ambalo amefanikiwa.

Taarifa rasmi kutoka Al Ahly inasema kuwa wamefikia makubaliano na staa huyo kuvunja mkataba huo uliosalia ambapo staa huyo alikosa nafasi kikosi cha kwanza punde tu baada ya kuondoka kwa kocha Pitso Mosimane ambaye alimsajili akitokea Simba sc.

Kimsingi Simba sc ilishakubaliana maslahi binafsi na staa huyo huku kikwazo kilikua jinsi ya kuvunja mkataba wake uliosalia na Al Ahly jambo ambalo limekamilika huku ikitajwa kuwa kati ya Pape Osman Sakho na Peter Banda mmoja atampisha staa huyo.

Kurejea kwa Luis Miquissone Simba sc anatarajia kuvuna zaidi ya dola za kimarekani laki Moja na Ishirini (1200000 USD) ambazo ni sawa za zaidi ya shilingi milioni mia mbili hamsini za kitanzania pamoja na mshahara unaokadiliwa kuwa Dollars Elfu 14 ambazo ni zaidi ya Million 30.

 

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala