Connect with us

Makala

Miloud Alamba Tuzo Aprili 2025

Kocha mkuu wa klabu ya Yanga sc Miloud Hamdi amechaguliwa kuwa kocha bora wa mwezi April wa ligi kuu ya Nbc nchini baada ya kupata matokeo bora zaidi kuzidi wapinzani wake katika michezo ya ligi kuu kwa mwezi huo.

Miloud amewashinda Aman Josiah wa Tanzania Prison na David Ouma wa Singida Black Stars ambao aliingia nao fainali katika tuzo hiyo.

Miloud aliyejiunga na Yanga sc akitokea Singida Black Stars aliingoza Yanga sc katika michezo minne iliyocheza mwezi huo akizifunga klabu za Tabora United 3-0,Coastal Union 1-0,Azam Fc 2-1 na Fountain Gate Fc 4-0.

Pia Kiungo wa ushambuliaji wa klabu ya Dodoma Jiji Fc Iddy kipagwile ameshinda tuzo hiyo ya mchezaji bora wa mweziAprili  huku akiwashinda Haruna Chanongo wa Tanzania Prison na Pacome Zouzoua wa Yanga sc.

Kipagwile katika michezo minne ya klabu hiyo alifunga mabao matatu na kutoa asisti tatu zilizomfanya kutwaa tuzo hiyo.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala