Connect with us

Makala

Mgunda Apewa U-bosi Simba sc

Kocha Juma Mgunda amekabidhiwa majukumu mapya ya mkurugenzi wa ufundi ndani ya klabu ya Simba sc ambapo atahusika na soka la vijana,wanawake na akiwa pia ni mshauri wa timu kubwa illiyo chini ya kocha mkuu Roberto Oliveira.

Mgunda ambaye alipata umaarufu katika soka enzi za kale kisha akahamia kwenye ukocha akifanya vizuri katika klabu ya Coastal Union ya jijini Tanga kisha akachukuliwa na Simba sc kurithi nafasi ya kocha Zoran Maki ambaye alipata dili jipya nchini Misri.

Mgunda licha ya kufanya vizuri na Simba sc akifanikiwa kuipeleka timu hiyo hatua ya makundi aliletewa kocha wa zamani wa Vipers Fc ya Uganda Roberto Oliveira ambaye alishika majukumu ya ukocha mkuu huku yeye akifanywa msaidizi na msimu huu kocha huyo amekuja na wasaidizi wake akiwaacha Mgunda na Matola ambaye amepelekwa timu ya Simba B.

Taarifa za Mgunda kukabidhiwa majukumu hayo bado hazijatoka rasmi japo tayari yeye mwenyewe ameshafahamishwa kuhusu majukumu yake hayo mapya.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in Makala